Ibn ´Uthaymiyn kuhusu watu kuitana “al-Hajj fulani”

Swali: Ni ipi hukumu ya msemo “Ee al-Hajj” na “bwana fulani”?

Jibu: Kusema “ee al-Hajj” bi maana akikusudia amekwishatekeleza hajj hakuna neno.

Kuhusu tamko bwana kunatakiwa kutazamwe ikiwa kweli anastahiki wasfu huu pasi na kuweka أل hakuna neno kwa sharti asiwe ni mtenda madhambi mazito wala kafiri. Akiwa ni mtenda madhambi mazito au kafiri basi hapo itakuwa haijuzu kumpachika neno ´bwana` isipokuwa aegemezewe watu wake. Kwa mfano bwana wa wana fulani au bwana wa vijana fulani.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (03/97)
  • Imechapishwa: 06/06/2017