Ibn ´Uthaymiyn kuhusu kunyoa nywele za miguuni na mikononi II

Swali: Kuondosha nywele za mikononi na miguuni kunazingatiwa ni pambo halali kwa mwanamke au kunazingatiwa ni kuyabadilisha maumbile ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala)?

Jibu: Bora mtu akibakize kile alichoumbiwa na Allaah kama kilivyo. Isipokuwa tu kile kilichoamrishwa na Shari´ah kukiondosha. Kama mfano wa nywele za kwapani, nywele za sehemu za siri na makucha. Hizi zinatakiwa kuondoshwa kwa sababu ya kufuata Shari´ah. Ama zile ambazo hakukupokelewa chochote katika Shari´ah kuhusu kuziondosha, bora ni kuzibakiza kama zilivyo na wala asizibadilishe. Lakini nywele za mikononi na miguuni zikiwa nyingi kiasi cha kwamba zikatoka nje ya kile kilichozoeleka na zikawa mbaya na zenye kuchukiza katika desturi za watu, basi hakuna neno wala ubaya kuzipunguza.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (05) http://binothaimeen.net/content/6679
  • Imechapishwa: 11/10/2020