Ibn ´Uthaymiyn kugusa msahafu bila twahara


Swali: Ni ipi hukumu ya kugusa msahafu bila ya twahara?

Jibu: Maoni yenye nguvu kuhusiana na kugusa msahafu ni kwamba haifai isipokuwa kwa twahara. Inahusiana na hadathi zote mbili; hadathi kubwa na hadathi ndogo. Kuhusu usomaji wa Qur-aan inafaa kwa ambaye ana hadathi ndogo na wala haifai kwa ambaye ana hadathi kubwa mpaka kwanza aoge. Haya ndio maoni yenye nguvu juu ya masuala haya. Wanachuoni wametofautiana juu ya masuala haya. Lakini maoni ninayoona yana nguvu ni yale uliyosikia kutoka kwangu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (77) http://binothaimeen.net/content/1767
  • Imechapishwa: 15/09/2020