Ibn ´Uthaymiyn akiwaponda Khawaarij wa leo


Swali: Tuna kundi la wanafunzi vijana Yemen ambao wana maneno mazito kuhusu wanachuoni wakubwa na yamewapata vijana wengine. Wanasema ikiwa ni pamoja na kwamba Shaykh al-Albaaniy ni kiongozi wa Irjaa´. Wanasema hali kadhalika kuhusu kamati ya Kibaar-ul-´Ulamaa hapa na kwamba wana Irjaa´ na hawajui mambo ya kisasa[1]. Tunapojadiliana na wao kwa masikitiko makubwa wanasema kuwa wao ni Ahl-us-Sunnah, Salafiyyuun na mfano wa hayo. Vipi mtu atatangamana na wao? Unasemaje kuhusu wao?

Jibu: Kuhusiana na maneno yao kuhusu wanachuoni, hayawadhuru wanachuoni chochote. Sijui kitu kinachoonesha kuwa Shaykh al-Albaaniy ni Murji-ah. Ni Salafiy, Sunniy na Muhaddith. Kuna wachache sana mfano wake leo.

Kuhusiana na kwamba kamati ya Kibaar-ul-´Ulamaa hapa na kwamba hawajui mambo ya kisasa, ni kama madai mengine yote. Mwenye kudai anatakiwa alete dalili na mpingaji ale kiapo. Je, wamejadiliana na wanachuoni hawa na kuona ya kwamba hawajui mambo ya kisasa. Msemo ”kutojua mambo ya kisasa (Fiqh-ul-Waaqiy´) ni msemo ambao umezushwa unaotoka kwa baadhi ya walinganizi. Ufahamu wenye kusifika ni kuwa na ufahamu katika Dini ya Allaah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Yule ambaye Allaah Anamtakia kheri basi Humfanya akaifahamu Dini.” (al-Bukhaariy (71)) na Muslim (1037))

Kuyafahamu mambo ya kisasa ni njia ya kumfanya mtu akapata picha juu ya suala fulani ambapo baadaye anaweza kulihukumu kwa mujibu wa Shari´ah.

Swali: Kuhusiana na jinsi ya kutangamana na vijana kama hawa?

Jibu: Kuhusiana na jinsi ya kutangamana nao ninaonelea kuwa muachane nao.

Swali: Una maanisha tuwapuuze?

Jibu: Kabisa! Kana kwamba ni watu wasiokuwepo. Lakini lau atakuja mtu mwingine na akataka kuzungumza kuhusu mada hii anasihiwe, kuamrishwa kumcha Allaah (´Azza wa Jalla) na kumkataza kuzungumzia juu ya kitu asichokijua.

Swali: Kuwatuhumu wanachuoni wakubwa kwamba wana Irjaa´ si dalili inayoonesha kuwa wamemili? Ninakumbuka kuwa baadhi ya wanachuoni wametaja kwamba Ibn Badraan al-Hanbaliy amesema kuwa baadhi ya Khawaarij walikuwa wakiwatuhumu Ahl-us-Sunnah kuwa wana Irjaa´.

Jibu: Ndio, ndio. Hili halina shaka! Kila mwenye kuwatuhumu watu wa kati na kati kuwa na Irjaa´, amemili katika fikira za Khawaarij.

Swali: Ana kauli na fikira zao?

Jibu: Ndio. Anakuwa na fikira za

(1) Tazama http://www.wanachuoni.com/content/wanachuoni-wetu-wana-elimu-ya-fiqh-ul-waaqi%C2%B4-na-shari%C2%B4ah

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://https//www.youtube.com/watch?v=CignsoTEGnA&feature=youtube_
  • Imechapishwa: 02/05/2018