Ibn Baaz kuhusu thawabu za kisomo cha Qur-aan kumfikia maiti

Swali: Kuna katika wanachuoni wenye kuonelea kuwa inafaa kuwasomea Qur-aan maiti na kwamba thawabu zake zinawafikia. Ni upi usawa katika hayo?

Jibu: Usawa ni kwamba haziwafikii. Shaykh Taqiyy-ud-Diyn amethibitisha kuwa hazimfikii pasi na mzozo. Kumsomea Qur-aan thawabu hazimfikii. Isitoshe haijuzu kuchukua malipo kwa jambo hilo. Kwa kuwa haikupokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yenye kuthibitisha kwamba thawabu zinamfikia. Yaliyothibiti ni kujikurubisha kwa swadaqah, hajj na ´umrah. Haya yanamfikia na yanawanufaisha wale maiti. Ama masuala ya kumsomea hakuna dalili juu ya hilo. Kuhusu kuwaombea du´aa kunawafaa. Kumethibiti dalili juu ya hilo na maafikiano ya waislamu. ´Ibaadah zimejengwa juu ya Qur-aan na Sunnah peke yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 43
  • Imechapishwa: 16/11/2016