Swali: Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ummah wangu utagawanyika mapote 73. Yote hayo yataingia motoni ila moja tu.”

Je Jamaa´at-ut-Tabliygh na Shirki (ushirikina) na Bid´ah zao, na al-Ikhwaan al-Muslimuun na makundi yao ya vyama (Tahazzub) na uasi wao kwa mtawala, je ni katika makundi haya 72 yaliyopotea?

Jibu: Ni katika wao. Ataekwenda kinyume na ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah anaingia katika mapote haya 72. Maana ya naneo lake “Watu wangu” ni wale wanaomuitikia Allaah na kumfuata. Ni makundi 73. Kundi lililookoka ni lile linalomfuata na yale yale alokuja nayo. Katika hayo makundi 72 kuna ambayo ni makafiri, watu wa bid´ah na waasi.

Muulizaji: Ina maana haya makundi mawili ni katika hayo makundi 72?

Ibn Baaz: Ndio. Ni katika hayo mapote 72 na Murji-ah na wengineo. Murji-ah na Khawaarij. Baadhi ya wanachuoni wanaona kuwa Khawaarij ni makafiri na wakati huohuo ni katika mapote hayo 72.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.rabee.net/show_book.aspx?id=834&pid=3&bid=42
  • Imechapishwa: 03/09/2020