Swali: Nawaona baadhi ya waswaliji wanaweka ncha ya vilemba vyao chini ya paji zao za uso wakati wamesujudu. Ni ipi hukumu ya kitendo chao hichi?

Jibu: Ikiwa haja imepelekea kufanya hivo, kwa mfano ardhi ni yenye baridi, joto kali au kufunika uchi wake, hapana neno kufanya hivo. Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walikuwa wakifanya hivo wakati wa haja. Lakini kukiwa hakuna haja bora ni kutofanya hivo na mswaliji abashiri ardhi kwa uso wake. Hivo ndivo alivokuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akifanya na Maswahabah zake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/158)
  • Imechapishwa: 23/10/2021