Swali: Je, inajuzu kuweka kipande cha chuma au ishara juu ya kaburi la maiti ambayo imeandikwa Aayah za Qur-aan na aidha jina la maiti na tarehe ya kufa kwake?

Jibu: Haijuzu kuandika juu ya kaburi la maiti; si Aayah ya Qur-aan wala kitu kingine. Si kwenye chuma, kwenye ubao wala kitu kingine. Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kupitia kwa Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Amekataza kulitia chokaa kaburi, kukaa juu yake na kulijengea.”

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

at-Tirmidhiy na an-Nasaa´iy wamezidisha kwa cheni ya wapokezi Swahiyh:

“… na kuandika juu yake.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (04/337) https://binbaz.org.sa/fatwas/901/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D9%84%D9%83%D8%AA%D8%A7%D8%A8%D8%A9-%D8%B9%D9%84%D9%89-%D8%A7%D9%84%D9%82%D8%A8%D9%88%D8%B1
  • Imechapishwa: 01/12/2019