Hukumu ya kuacha sijda ya kusahau


Swali: Niliswali na imamu na nilikuwa nimekuja nimechelewa Rak´ah moja. Imamu alipotoa Tasliym nami nikatoa Tasliym hali ya kusahau. Papo hapo baada ya swalah nilipokumbuka nikakamilisha swalah yangu. Lakini sikusujudu sijda ya kusahau. Je, juu yangu kuna kitu?

Jibu: Ikiwa uliacha sijda ya kusahau kwa makusudi, basi swalah yako ni batili. Na ikiwa uliiacha kwa kusahau, basi unatakiwa kusujudu pale utakapokumbuka na hivyo swalah yako ni sahihi. Ingawa baadhi ya wanazuoni wanaona kuwa kukishapita muda kitambo kirefu au wudhuu´ wako ukachenguka basi sijda [ya kusahau] inadondoka.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (21)
  • Imechapishwa: 08/08/2021