Hekima ya Allaah katika kumkadiria mtu maasi

Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ فَزَادَهُمُ اللَّـهُ مَرَضًا ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْذِبُونَ

“Ndani ya nyoyo zao yamo maradhi na Allaah akawazidishia maradhi na watapata adhabu iumizayo kwa waliyokuwa wakiyakadhibisha.”[1]

Hapa kuna ubainifu wa hekima ya Allaah katika kuwakadiria maasi watenda maasi na kwamba kutokana na dhambi zao zilizotangulia ndio maana akawatahini kwa maasi yaliyowapata yatayosababisha wao kuadhibiwa. Amesema (Ta´ala):

وَنُقَلِّبُ أَفْئِدَتَهُمْ وَأَبْصَارَهُمْ كَمَا لَمْ يُؤْمِنُوا بِهِ أَوَّلَ مَرَّةٍ

”Tunazigeuza nyoyo zao na macho yao kama ambavo hawakuiamini mara ya kwanza.”[2]

فَلَمَّا زَاغُوا أَزَاغَ اللَّهُ قُلُوبَهُمْ

“Pale walipopondoka basi ndipo Allaah akazipondoa nyoyo zao.”

وَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ مَرَضٌ فَزَادَتْهُمْ رِجْسًا إِلَى رِجْسِهِمْ

”Ama wale ambao katika nyoyo zao mna maradhi, basi huzidishiwa rijisi juu ya rajisi yao.”[3]

Adhabu ya maasi ni maasi mengine baada yake kama ambavo thawabu za tendo jema ni tendo jema jengine baada yake. Ameema (Ta´ala):

وَيَزِيدُ اللَّهُ الَّذِينَ اهْتَدَوْا هُدًى

“Awazidishie Allaah wale waliooongoka uongofu.”[4]

[1] 02:10

[2] 06:110

[3] 09:125

[4] 19:76

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taysiyr-ul-Kariym, sid. 32
  • Imechapishwa: 08/05/2020