01. Hadiyth “Yule anayehifadhi Rak´ah nne kabla ya Dhuhr… “

584- Umm Habiybah (Radhiya Allaahu ´anhumaaa) amesimulia kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Yule anayehifadhi Rak´ah nne kabla ya Dhuhr na nne baada yake, Allaah atamharamishia Moto.”[1]

Ameipokea Ahmad, Abu Daawuud, an-Nasaa’iy na at-Tirmidhiy kupitia kwa al-Qaasim Abu ´Abdir-Rahmaan, Swahabah wa Umm Umaamah, kutoka kwa ´Anbasah bin Abiy Sufyaan, kutoka kwa Umm Habiybah. at-Tirmidhiy amesema:

“Hadiyth ni nzuri, Swahiyh na geni. al-Qaasim ni mwana wa ´Abdur-Rahmaan na kun-ya yake ni Abu ´Abdir-Rahmaan. Ni mtu wa Shaam na ni mwaminifu.”

[1] Nzuri na Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/380)
  • Imechapishwa: 08/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy