Hedhi iliyompata mwanamke katika wakati wa swalah


Swali: Mwanamke akipata hedhi mwanzoni mwa [kuingia kwa] wakati. Je, wakati hedhi yake itaisha na kutwahirika atalipa swalah hii?

Jibu: Hapana, hatoilipa.

Swali: Kadhalika mwanamke akipata hedhi mwishoni mwa wakati [wa swalah] na alikuwa bado hajaswali [swalah hii]. Je, atalipa swalah hii?

Jibu: Ndio. Hili lina haki zaidi. Akichelewesha swalah mpaka mwisho wa wakati wa pili – na sio mwishoni mwa wakati wa mwanzo – akapatwa na hedhi, anatakiwa kulipa swalah mbili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13342
  • Imechapishwa: 20/09/2020