Hatumshuhudilii yeyote Pepo wala Moto

Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:

“Hatumshuhudii muislamu yeyote kwa kitendo alichofanya kuingia Peponi wala Motoni.”

Bi maana midhali dhambi sio kufuru. Ikiwa dhambi ni kufuru au shirki, ina hukumu yake. Ama dhambi ikiwa ni maasi tu, hatumshuhudilii Pepo wala Moto. Akifanya matendo mema tunatarajia kwake Pepo. Akifanya matendo yanayopelekea katika Moto, tunachelea kwake. Tunatarajia kwa yule mwenye kutii na tunachelea kwa mtenda maasi. Hatumkatii yeyote Pepo wala Moto. Hakuna mwenye haki ya kufanya hivo isipokuwa Allaah (´Azza wa Jall) peke yake. Isipokuwa tu kufuru ya wazi. Myahudi au mnaswara ni makafiri, ni jambo liko wazi. Mtu kama huyu ataingia Motoni. Tunashuhudia ya kwamba kafiri ataingia Motoni. Ni muumini, ambaye ni mtenda maasi au mwenye kutii, ndiye ambaye hatumshuhudilii si Pepo wala Moto. Jambo lake liko kwa Allaah (´Azza wa Jall). Tunamtarajia yule mwenye kutii na tunachelea kwa yule mwenye kuasi. Tunatarajia kwa yule mwema na wakati huo huo tunachelea juu yake. Kwa sababu kuna uwezekano anafanya matendo mema kwa uinje na kwa undani ni kinyume kabisa na hivo.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah, uk. 431
  • Imechapishwa: 25/07/2017