Hatufungui mlango wa suruwali kwa mwanamke


Swali: Dada huyu anauliza. Ni ipi hukumu kwa mwanamke kuvaa suruwali mbele ya watoto na akiwa na mume wake tu?

Jibu: Akiivaa mbele ya watoto atakuja kuivaa hata mbele ya wakubwa. Sisi hatufungui mlango na nafasi. Haijuzu kwake kuivaa anapokuwa na mume wake. Tukifungua mlango huu na kusema kuwa inajuzu, tutakuwa tumefugua mlango na itakuwa sasa ni vazi la wanawake. Na khaswa wakati wa sasa ambapo watu wamekabiliwa na kuiga na kujifananisha na wasiokuwa sisi. Tunasema “Hapana”, mwanamke aisitiri nafsi yake kwa nguo na mavazi yake na himdi zote ni stahiki ya Allaah. Amshukuru Mola Wake kwa hilo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13267
  • Imechapishwa: 07/09/2020