Hapa ndipo unaruhusiwa kumuuliza mwanachuoni mwingine

Swali: Kuna mwanachuoni nilimuuliza maswali fulani ambapo akanijibu kwamba haijuzu. Ndani ya moyo wangu kukabaki kitu juu ya jawabu lile. Kisha nikaenda kwa mtu ambaye najua kuwa ni mjuzi na msomi zaidi kulikoni na elimu yake imeshuhudiwa ambapo nikamuuliza swali lilelile na akajibu kwamba inajuzu. Je, kitendo changu hichi kinaingia katika kufuatafuata ruhusa?

Jibu: Ikiwa muulizaji huyu hakupata utulivu wa jibu la yule aliyemuuliza kwa sababu halijaendana na matamanio yake na matokeo yake ndio akamuuliza mwingine, huku ni kufuata ruhusa. Ama ikiwa hakupata utulivu kwa kudhani kwamba huku ni kwenda kinyume na Shari´ah ni sawa akauliza na akawa na uslama zaidi juu ya dini yake. Masuala haya yanahitajia upambanuzi. Wakati fulani mtu hahisi utulivu juu ya fatwa ya mwanachuoni kwa sababu haiendani na matamanio yake. Huyu kwake si halali kumuuliza mwingine. Wakati mwingine unadhani kuwa amekosea na usawa unapatikana katika maoni mengine, katika hali hii ni sawa ukamuuliza mwingine katika wale ambao unaona kuwa ni wajuzi zaidi kulikoni.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (42) http://binothaimeen.net/content/974
  • Imechapishwa: 12/12/2018