Swali: Baadhi ya wanafunzi wanakosoa baadhi ya makosa ya wanachuoni ambapo baadae wanayaeneza kati ya watu na wanasema kuwa ni Jarh na Ta´diyl. Je, kitendo chake ni sahihi?

Jibu: Mmekariri swali hili kuhusu Jarh na Ta´diyl. Jarh na Ta´diyl ni elimu kuhusu mlolongo wa wapokezi wa Hadiyth. Jarh na Ta´diyl haiwahusu watu wasiopokea Hadiyth na wala hawana mafungamano yoyote na Hadiyth. Huku ni kusengenya na kueneza uvumi. Sio Jarh na Ta´diyl. Huku ni kusengenya ambako hakujuzu. [Inajuzu tu] ikiwa mtu huyu madhara yake ni yenye kuenea kwa wengine na anasababisha wengine kupotea. Katika hali hii ni wajibu kubainisha hali yake na kutahadharisha nae.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (07) http://alfawzan.af.org.sa/node/2050
  • Imechapishwa: 27/12/2016