Hakuna haja ya kutaja jina la unayemchinjia na du´aa ya kuchinja

Akimchinja katika ´Iyd-ul-Adhwhaa na akamnuia yule mwenye kuchinjiwa pasi na kumtaja kwa jina inatosheleza. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika kila kitendo kinategemea na nia na kila mmoja atalipwa kwa vile alivyonuia.”[1]

Tasmiyah iiliyosuniwa ni yeye kusema wakati wa kuchinja:

بسم الله والله أكبر، اللهم هذا عني وعن أهلي

“Kwa jina la Allaah, Allaah ni mkubwa. Ee Allaah! Hiki [kichinjwa] ni kwa ajili yangu na familia yangu.”

au maneno mfano wa hayo.

Yale yanayofanywa na baadhi ya watu wajinga ambapo wanagusa mgongo wa mnyama yule hali ya kukariri jina la anayechinjiwa, sijui msingi wowote wa jambo hilo na hivyo haitakiwi kufanya hivo. Kwa sababu uongofu bora ni wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] al-Bukhaariy (01) na Muslim (1907).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (25/162-163)
  • Imechapishwa: 29/07/2020