Swali: Kasema Shaykh-ul-Islaam bin Taymiyyah katika kitabu chake “Iqtidhwaa´ as-Swiraat al-Mustaqiym” kuwa ni Ijmaa´ kwa mwenye kumtukana Mtume yeyote katika Mitume wakati wa utume wake kuwa ni kafiri. Je kumtukana Mtume yeyote hukumu yake ni katika mambo yanayojulikana na kila mtu na mtu huyo anakuwa kafiri au ni katika mambo ambayo yanaweza yakawa hayako wazi na akapewa mtu huyo udhuru kwa ujinga?

Jibu: Kamwe! Mwenye kumtukana Mtume karitadi anauawa na wala haambiwi kutubia. Hili ni kwa Ijmaa´. Anauawa wala haambiwi kutubia, anakuwa karitadi kutoka katika dini ya Uislamu. Wala hakuna yeyote asiyejua hili. Hili hakuna yeyote asiyelijua. Kuna yeyote asiyejua kuwa kumtukana Allaah ni kufuru? Hali kadhalika kwa mwenye kuwatukana Mitume (´alayhim-us-Swalaatu was-Salaam). Hakuna asiyejuwa kuwa kuwatukana ni kufuru na ilhadi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.ws/node/2819 Tarehe: 1431-05-13/2010-04-26
  • Imechapishwa: 10/04/2022