Tunasema bila shaka kutafuta elimu ya Kishari´ah ni katika bora ya matendo mema. Bali linakwenda sambamba na Jihaad katika njia ya Allaah. Kama alivyosema Allaah (Tabaarak wa Ta´ala):

وَمَا كَانَ الْمُؤْمِنُونَ لِيَنفِرُوا كَافَّةً ۚ فَلَوْلَا نَفَرَ مِن كُلِّ فِرْقَةٍ مِّنْهُمْ طَائِفَةٌ لِّيَتَفَقَّهُوا فِي الدِّينِ وَلِيُنذِرُوا قَوْمَهُمْ إِذَا رَجَعُوا إِلَيْهِمْ لَعَلَّهُمْ يَحْذَرُونَ

“Na haiwapasi waumini watoke wote pamoja kwenda [kupigana vita vya jihaad]. Basi kwanini lisitoke katika kila kundi miongoni mwao, kundi [moja] wajifunze dini na ili waonye watu wao watakaporejea kwao ili wapate kutahadhari.” (09:122)

Kabainisha Allaah (´Azza wa Jall) kuwa waumini haiwezekani wakaenda wote kwenye Jihaad katika njia ya Allaah, kwa kuwa hilo linapelekea mambo mengi muhimu yote husimama ambayo Uislamu inapaswa kusimama nayo.

Kutokana na hili tunapata kujua kuwa Jihaad haiwezi kuwa fardhi ‘Ayn kwa kila Muislamu kama wanavyodai baadhi ya watu leo kuwa Jihaad ni fardhi ‘Ayn kwa kila muislamu. Hili ni kosa linakhalifu Qur-aan. Kwa kuwa Allaah kasema:

وَمَا كَانَ الْمُؤْمِنُونَ لِيَنفِرُوا كَافَّةً

“Na haiwapasi waumini watoke wote pamoja kwenda [kupigana vita vya jihaad].”

Kisha akaamrisha waende baadhi yao na wengine wabaki ili waisome dini ya Allaah na wawaonye wenzao watakaporejea. Lakini Jihaad inakuwa Fardhi ‘Ayn katika masuala khaswa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (164 A)
  • Imechapishwa: 10/04/2022