Haitakiwi kuwasifu makafiri


Swali: Je, inajuzu kuwasifu makafiri na kuzungumza lugha yao pasi na haja?

Jibu: Haijuzu kuwasifu. Hawatakiwi kusifiwa. Kinyume chake inatakiwa kubainisha ile shirki na kufuru waliyomo, kutahadharisha matendo yao na kujitenga nao mbali.

Kuhusu kuzungumza lugha yao inatakiwa iwe wakati wa haja, kama kulingania katika dini ya Allaah na kipindi mtu analazimika kufanya hivo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alharamain.gov.sa//index.cfm?do=cms.AudioDetails&audioid=63284&audiotype=lectures&browseby=speaker
  • Imechapishwa: 26/08/2017