Haijuzu kuwa na rafiki anayetangamana na Ahl-ul-Bid´ah


Swali: Rafiki yangu anakaa na Ahl-ul-Bid´ah na anawatetea na nimeshamnasihi. Je, nimsuse ili ajirudi na upi muda wa kumsusa?

Jibu: Rafiki yako akiendelea kukaa na Ahl-ul-Bid´ah na kutangamana nao, siyo halali kwako kumfanya rafiki. Mfano wa kukaa na mtu mwema na muovu ni kama mfano wa muuza miski na mtu mwenye kupuliza moto. Mpe chaguo. Ima aache kukaa na watu wa Bid´ah na upotofu au ufarakane nae.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin Swaalih al-Luhaydaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=129510
  • Imechapishwa: 10/04/2022