Haijuzu kumtaliki mwanamke wa nifasi na hedhi


Swali: Je, inajuzu kumtaliki aliye na nifasi ndani ya muda wa nifasi?

Jibu: Talaka haijuzu ndani ya muda wa nifasi wala hedhi. Kwa Kauli Yake (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَطَلِّقُوهُنَّ لِعِدَّتِهِنَّ وَأَحْصُوا الْعِدَّةَ

“Ee Nabii! Mtakapowataliki wanawake, basi watalikini katika wakati wa eda (twahara na si katika hedhi) zao.” (65:01)

Yaani wakiwa Twahara bila ya kuwagusa. Hii ndio maana ya “li´addatihinna”.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/10051
  • Imechapishwa: 05/03/2018