Haifai kusimamisha adhabu za Kishari´ah bila idhini ya mtawala

Swali: Inajuzu kwa mtu binafsi kumuua mchawi kutokana na aliyoyafanya Swahabah mtukufu Jundub bin Ka´b (Radhiya Allaahu ´anh) au ni lazima kupewa idhini na mtawala?

Jibu: Jundub ni Swahabah. Maswahabah wana sifa za kipekee pasi na wengine. Haijuzu kumuua mchawi au kusimamisha adhabu zengine isipokuwa kwa amri ya mtawala. Haijuzu kufanya hivi isipokuwa kwa amri ya mtawala. Kuhusu aliyoyafanya Jundub ni katika matendo ya Maswahabah. Maswahabah wana sifa za kipekee wasizokuwa nazo wengine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam (07) http://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/07.mp3
  • Imechapishwa: 11/01/2019