Furahikia neema za ndugu yako na usimhusudu

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hasadi inakula mema [ya mtu] kama jinsi moto unavokula kuni.”

Mtu kuwa na hasadi haikomeki kwa mtu kupata dhambi peke yake, bali ni kwamba hasadi inaondosha mema ya mwenye kufanya hivo. Kwa sababu hasadi inahusisha imani mbovu kwa kumfikiria vibaya Allaah (Jalla wa ´Alaa) kwa kule kuingiwa kwenye moyo wake kwamba huyu aliyepewa hastahiki kupewa fadhila na neema za Allaah (Jalla wa ´Alaa) Zake. Mfano wa jambo hili hufanywa na wale watu wjinga pale wanaposema:

“Huyu imeharamishwa kwake kupewa kadhaa na kadhaa.”

“Ni haramu kwa mtu huyu kuwa na neema hii.”

“Ni haramu kwa mtu huyu kuwa na mali hii.”

Na matamshi mengineyo ambayo ndani yake kuna kumdhania vibaya Allaah (Jalla wa ´Alaa) na kupingana na Qadar, neema na riziki Yake Anayoigawanya vile Anavotaka.

Lililo la wajibu kwa muislami ni afurahie neema za ndugu yake ambazo Allaah amemtunukia.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 480
  • Imechapishwa: 12/05/2020