Fidia ya adhabu juu ya kazi inayocheleweshwa

Swali: Nilimwomba mkandarasi anijengee nyumba na tukapangiana muda wa miezi minne. Tukaafikiana juu ya hilo na kwamba akipitisha muda huo basi atalipa fidia ya kiwango cha SAR 500 kwa kila siku moja inayopita. Hivi sasa kumeshapita mwaka mzima. Je, inafaa kwangu kuomba fidia?

Jibu: Haifai kufanya hivo ikiwa ana waajiri wengi. Katika hali hii haifai kuiwekea kazi hiyo kikomo cha muda, kwa sababu kazi inaweza kuwa ngumu na inahitajia muda. Haifai kuiwekea kazi hiyo kikomo cha muda. Lakini akiwa hana kazi nyingine isipokuwa yako tu na akachelewesha pasi na udhuru, ada hii inaitwa fidia ya adhabu. Inafaa kuomba fidia ya adhabu juu ya kazi inayocheleweshwa pasi na udhuru kwa sababu ya kumlinda mwajiri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (28)
  • Imechapishwa: 04/02/2022