Kadhalika tumebainisha maana ya maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“… na kuswali katikati ya usiku.”

Kusimama usiku ni jambo limependekezwa. Ni jambo lina daraja mbali mbali. Daraja iliyo juu kabisa ni kama ile ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) iliyokuja mwishoni mwa Suurah “al-Muzzammil”:

إِنَّ رَبَّكَ يَعْلَمُ أَنَّكَ تَقُومُ أَدْنَىٰ مِن ثُلُثَيِ اللَّيْلِ وَنِصْفَهُ وَثُلُثَهُ وَطَائِفَةٌ مِّنَ الَّذِينَ مَعَكَ

“Hakika Mola wako Anajua kwamba unasimama [kuswali] karibu na thuluthi mbili za usiku na [wakati mwengine] nusu yake, na [wakati mwengine] thuluthi yake; na kundi miongoni mwa wale walio pamoja nawe [pia linasimama kuswali].” (73:20)

Kisimamo ambacho ni bora ni kile kinachoanza baada ya katikati ya usiku mpaka alfajiri. Cha kufuata ni kile kinachokuwa mwanzoni wa thuluthi ya mwisho ya usiku mpaka alfajiri kisha daraja inaendelea hivo kwa kiasi na itakavyomkuwia mtu sahali.

Mtu kusimama katikati ya usiku ni miongoni mwa milango mikubwa ya kheri. Mtu hupata nuru ndani ya moyo wake kwa kufanya hivo, kutangamana na Mola Wake kwa uzuri, kumcha Allaah, kuipa nyongo dunia na kuipupia Aakhirah kiasi cha kwamba haiwezi kuelezeka. Allaah Atusaidie sisi na nyinyi kwa hilo.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 408
  • Imechapishwa: 14/05/2020