Swali: Tunaomba utueleze kuhusu fadhilah za kutumia Siwaak na nyakati zake?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu fadhilah za Siwaak:

Siwaak ni yenye kumridhisha Mola na ni yenye kusafisha mdomo.”

Hizi ni faida mbili kubwa:

Ya kwanza: Usafi wa kihisia. Nako ni kule kuusafisha mdomo kutokamana na uchafu. Unsafisha meno, mafizi na ulimi.

Ya pili: Nayo ndio faida kubwa. Ni kwamba Siwaak inamridhisha Mola (´Azza wa Jall).

Katika Hadiyth hii kuna mahimizo ya Siwaak kutokana na kutajwa kwa faida mbili ya duniani na ya Aakhirah. Faida ya duniani ni kuusafisha mdomo. Faida ya Aakhirah ni kumridhisha Mola (´Azza wa Jall). Kitu kingine kinachofahamisha fadhilah zaek ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Lau nisingeliwaonea huruma Ummah wangu basi ningeliwaamrisha Siwaak wakati wa kila swalah.”

Bi maana angeliwaamrisha amri ya ulazima. Kitu hakiwajibishwi isipokuwa kwa manufaa makubwa yaliyopelekea watu walazimishwe nayo. Lakini manufaa haya makubwa yamepelekea katika uzito mkubwa uliyochelewa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya Ummah wake na ndio maana akaacha kuwalazimisha jambo hilo.

Kuhusu sehemu za Siwaak zilizokokotezwa:

1- Kabla ya kutawadha. Mahali pake ni wakati wa kusukutua. Ni sawa pia endapo atachelewesha kutumia Siwaak mpaka wakati mtu atapomalia kutawadha. Yote mawili ni sawa.

2- Kabla ya kuswali. Ni mamoja swalah hiyo ni ya faradhi au ni ya sunnah. Ni mamoja swalah hiyo ina Rukuu´ na Sujuud au haina Rukuu´ na Sujuud kama mfano wa swalah ya jeneza.

3- Wakati mtu anapoamka kutoka usingizini. Hakika imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba mtu anapoamka kutoka usingizini basi apige Siwaak mdomoni mwake.

4- Wakati mtu anapoingia nyumbani. Hakika Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kitu cha kwanza alichokuwa anaanza nacho ni kutumia Siwaak.

Mbali na nayakati hizo Siwaak imesuniwa katika kila wakati. Lakini imekokotezwa katika nafasi hizi nne.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (263) http://binothaimeen.net/content/10582?q2=%D9%88%D9%82%D8%AA%20%D8%A7%D9%84%D8%B3%D9%88%D8%A7%D9%83%20%D9%88%D9%85%D8%A7%20%D8%AC%D8%A7%D8%A1%20%D9%81%D9%8A%20%D9%81%D8%B6%D9%84%D9%87
  • Imechapishwa: 29/02/2020