Eti haifai kwa mwenye hedhi kuosha kichwa chake?

Swali 126: Ni ipi hukumu mwanamke mwenye hedhi kuosha kichwa chake wakati wa hedhi? Kwani wako ambao wanasema kuwa haifai.

Jibu: Hakuna neno kwa mwanamke mwenye hedhi kuosha kichwa chake wakati wa hedhi. Maneno yao kwamba haifai hayana usahihi wowote. Hivyo inafaa kwake kuosha kichwa chake na mwili wake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 54
  • Imechapishwa: 31/08/2019