Dini yote katika al-Arba´iyn an-Nawawiyyah    

Hadiyth hizi arubaini za an-Nawawiy – ambazo zimezidishwa juu yake vilevile – mna elimu ya Dini yote. Hakuna jambo lolote miongoni mwa mambo ya Dini ispokuwa yanapatikana katika Hadiyth hizi, sawa ikiwa ni katika ´Aqiydah au Fiqh. Hili litabainika kwa yule aliyesoma Sharh ya ajabu ya Ibn Rajab (Rahimahu Allaah) juu ya Arba´iyn an-Nawawiyyah na Hadiyth ambazo alizidisha kisha akazisherehesha. Kuzifahamu ni muhimu kwa kuwa katika kuzifahamu kuina kufahamu msingi wa Shari´ah kwa jumla na kanuni za Dini. Hakika juu yake kuna Hadiyth ambazo zimezunguka Ahkaam, kama itavokuja ubainifu wake – Allaah akitaka – kwa ufafanuzi.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawyyah, uk. 09
  • Imechapishwa: 10/05/2020