Da´wah ya az-Zindaaniy katika Tawhiyd inahusiana tuu na Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah

Swali: Ni yapi maoni yako kuhusu kitabu cha Tawhiyd cha az-Zindaaniy na unapendekeza mtu kukisoma?

Jibu: Mtu huyu alinipa kitabu hichi nilipokuwa Makkah na wakati huyo nilikuwa nasoma hapa na akaniuliza maoni yangu juu ya kitabu hichi, nikamwambia amechothibitisha ni Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah tu. Iko wapi Tawhiyd-ul-´Ibaadah na Tawhiyd-ul-Asmaa´ was-Swifaat? Akanyamaza. Halafu nikasafiri kwenda Yemen mimi na baadhi ya marafiki zangu na ninakutana naye huko na nikamkumbusha qadhiya hii ya kwamba ameishia katika kitabu chake cha Tawhiyd kuzungumzia Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah tu na ilihali Mitume wote walitumwa kwa lengo la kufikisha Tawhiyd-ul-Ilaahiyyah kwa kuwa watu katika kila zama na mahala ni wenye kuikubali Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=26881
  • Imechapishwa: 19/05/2015