Swali: Siku moja ya Ramadhaan na takriban robo saa kabla ya kuzama kwa jua nilipangusa meno yangu kwa kitambaa ambapo nikatokwa na damu na mimi sikuwa mwenye kukusudia kufanya hivo. Nina ugonjwa huu tangu hapo zamani pale ambapo ninaswaki basi natokwa na damu. Je, swawm yangu ni sahihi?

Jibu: Ndio, swawm yako ni sahihi. Damu hii inayotoka kwenye fizi za mtu wakati wa kupanguza au wakati wa kuswaki haidhuru swawm yake.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdullaah bin Ghudayyaan

´Abdullaah bin Qu´uud

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah nr. (3785)
  • Imechapishwa: 28/04/2022