Bora Adhkaar zifanywe kwa mkono wa kulia II

Swali: Mtu anaweza kusema kwamba kuleta Adhkaar kwa mikono miwili ndio bora zaidi kuliko kuleta Adhkaar kwa mkono wa kulia peke yake kwa sababu kuleta kwa mikono miwili ndani yake kuna amri na kuleta kwa mkono wa kuume ni kitendo?

Jibu: Jambo ni lenye wasaa. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anapenda kuanza kwa upande wa kulia wakati wa kuvaa kwake viatu, kuchana nywele zake, kujitwahirisha kwake na katika mambo yake yote.”

Imekuja katika Hadiyth iliopokea at-Tirmidhiy na wengineo:

“Alikuwa akifanya Tasbiyh kwa mkono wa kuume.”

Vilevile alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiwaamrisha baadhi ya wakeze kuhesabu kwa vidole, jambo ambalo linajumuisha mikono yote miwili. Kwa hivyo jambo ni lenye wasaa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21636/هل-التسبيح-باليدين-افضل-ام-باليمين-وحدها
  • Imechapishwa: 01/09/2022