Barua ya Jibriyl kwenda kwa Ahmad an-Najmiy

[Baada ya salamu za kidugu na utangulizi…

Unasema katika barua yako:

”Nimepata kitabu chako “al-Mawrid al-´Adhb az-Zulaal fiymaa intuqida ´alaa ba´dhw-il-Manaahij ad-Da´wiyyah min al-´Aqaa´id wal-A´maal”. Nilifurahishwa na kichwa cha khabari hichi chenye kuvutia ambacho kilinifanya kutaka kusoma kitabu chote. Mwanzoni nilifikiri kuwa ni maudhui yenye faida kuhusiana na kulingania katika Tawhiyd na mifumo ya Da´wah.

Nilipofika kwenye mlango wa tisa, nilikutana na kitu ambacho sikukitarajia kutoka kwa mtu kama wewe. Inahusiana na kumsema vibaya Hasan al-Bannaa. Unamshambulia na kufasiri maneno yake kimakosa.”

Miaka kumi iliyopita nilipata khabari kuhusu mtu huyu kutoka kwa wanachuoni waheshimiwa kama Shaykh ´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy, Shaykh ´Abdur-Rahmaan ad-Dawsaariy, Shaykh ´Abdullaah bin Humayd, Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz na watu mfano wao. Walichunguza kisa chake na kumpa udhuru kwa makosa aliyotumbukiaemo. Walikuta maneno yake yanaashiria kuwa alikuwa ni mtu mwenye Ikhlaasw na mpwekeshaji. Allaah amenufaisha watu kwa ulinganizi wake na amewaongoza watu wengi kupitia kwake. Nyakati zote anasifiwa katika vikao na vitabu vyake vinasomwa.

Lakini tangu miaka saba ya nyuma ndugu wengi wamemshambulia na kumpokonya haki yake. Haieleweki kabisa. Kuna vitabu vinavyojulikana ambavyo ni vibaya zaidi kuliko vitabu vyake. Kuna walinganizi, walio hai maiti, waliopinda zaidi kuliko yeye.

Hivyo basi, mimi nakunasihi, ee Shaykh, kuchunga ulimi wako na kumzungumza vibaya mtu huyu ambaye Allaah amewanufaisha na kuwaongoza wengi kupitia yeye. Usichapishe kitabu hiki ambacho kitakuja kukupa tetesi mbaya na kukufanya kusema vibaya heshima ya ndugu yako muislamu. Nasikitika siwezi kukutumia nuskha [uliyonitumia] kwa sababu nimeiwekea taaliki ambayo sitaki ije kuonekana. Allaah akitujaalia kuweza kukutana, basi natumai majadiliano ya kimdomo.

´Abdulaah bin ´Abdir-Rahmaan al-Jibriyn

Mjumbe wa Daar-ul-Iftaa´ wad-Da´wah wal-Irshaad.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Radd-ul-Jawaab, uk. 6-13
  • Imechapishwa: 02/07/2020