[Baada ya salamu za kidugu na utangulizi…

Unasema kwenye barua yako:

“Nimepata kitabu chako “al-Mawrid al-´Adhb az-Zulaal fiymaa intuqida ´alaa ba´dhw-il-Manaahij ad-Da´wiyyah min al-´Aqaa´id wal-A´maal”. Nilifurahishwa na kichwa cha khabari hichi chenye kuvutia ambacho kilinifanya kutaka kusoma kitabu chote. Mwanzoni nilifikiri kuwa ni maudhui yenye faida kuhusiana na kulingania katika Tawhiyd na mifumo ya Da´wah.

Nilipofika kwenye mlango wa tisa, nilikutana na kitu ambacho sikukitarajia kutoka kwa mtu kama wewe. Inahusiana na kumsema vibaya Hasan al-Bannaa. Unamshambulia na kufasiri maneno yake kimakosa.”

Nilisikitika pindi niliposoma barua yako na vipi inaweza kutoka kwa mtu kama wewe ulie na elimu na nafasi kama ulonayo.

Lau ungeliendelea kusoma na kuona kama nimesema haki au batili. Ikiwa ni haki, basi ungetakiwa kunisapoti kutokana na maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mnusuru ndugu yako sawa akiwa ni mwenye kudhulumu au mwenye kudhulumiwa.” Kukasemwa: “Tunajua anavyonusuriwa akiwa ni mwenye kudhulumiwa, vipi ananusuriwa ikiwa ni mwenye kudhulumu?” Akasema: “Mzuie na dhulumu yake.”

Na ikiwa nimesema batili, basi utanisaidia kwa kunibainishia haki kwa dalili na hoja. Niko tayari kupokea hilo kutoka kwako. Nitakushukuru kwa hilo na kukuombea du´aa kwa kuwa utakuwa umeniokoa kutokamana na dhambi na dhuluma ambayo nitakuwa nimetumbukiemo. Hata hivyo nina sharti. Nataka uje na ukosoaji uliofafanulia ulio na hoja na dalili za wazi kabisa zenye kubainisha kosa langu.

Ama kufika tu kwenye mlango wa tisa kisha unaacha kusoma na kunishambulia tu pasi na dalili yoyote, hili ni jambo ambalo sikukubalii. Kamwe sintoafikiana na wewe.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Radd-ul-Jawaab, uk. 5-6
  • Imechapishwa: 02/07/2020