Swali: Tunataka nasaha juu ya Radd kwa kila utata au fatwa yenye kwenda kinyume na Shari´ah ikiwa ni pamoja vilevile na wale wenye kuhalalisha kusherehekea Maulidi?

Jibu: Ni jambo lisilokuwa na shaka ya kwamba nasaha na ubainifu ni wajibu na khaswa kunapodhihiri fitina, Bid´ah na mambo ya kuzua katika zama za mwisho. Hapo ndipo inakuwa wajibu zaidi kwa wanachuoni wasimamie wajibu wao kwa watu na viumbe. Allaah amewabebesha wanachuoni amana wawafikishie nayo watu na wasiifiche. Kila ambaye ana elimu ni wajibu kwake kuifikisha na kukataza uhalifu unaotokea kwa watu, matendo na mienendo. Haitakiwi kwa mwanachuoni kunyamazia matendo ya watu hata kama watamtuhumu kuwa na haraka, msimamo mkali na mengineyo. Awe na subira juu ya hili.

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com