Baadhi ya misingi ya Haddaadiyyah 01


Nimesoma makala iliyoandikwa na mtu anayejiita yeye mwenyewe “Fawziy al-Athariy” inayoitwa “ar-Ruduud as-Swawaa´iqiyyah li Swa´q alfaadhw Rabiy´ al-Madkhaliy al-Bid´iyyah”. Makala yake ameijaza uongo na kuyapotosha maneno ya maimamu na wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah kwa kuyahamisha kutoka katika mazingira yake na kuyakariri ili makala yake yenye kutia aibu ionekane kuwa ni kubwa ili Haddaadiyyah waseme kuwa ni mwanachuoni na ni msomi.

Kabla ya kuanza kuijadili makala hii ninaonelea kuwa ni haki ya msomaji aweze kupata taswira ya haraka juu ya Haddaadiyyah wapya na misingi yao na mafungamano yao na Haddaadiyyah wa zamani ili upotevu na udanganyifu wao ubainike kwa watu:

1- Msingi mkubwa wa Haddaadiyyah ni kuwatuhumu Ahl-us-Sunnah Irjaa´. Haddaadiyyah wa leo wanawapiga vita Ahl-us-Sunnah kwa Irjaa´ vibaya sana mara kumi kuliko wahenga wao walivyokuwa wakifanya.

2- Moja katika misingi mikubwa ya Haddaadiyyah ilikuwa ni kuwapiga vita Ahl-us-Sunnah. Haddaadiyyah wa leo wanafanya vita mbaya sana na wanahimiza zaidi katika hilo.

3- Wanamfanyia Tabdiy´ kila mmoja katika Ahl-us-Sunnah anayetumbukia katika kitu katika Bid´ah. Haddaadiyyah wa leo pia wanafanya hivo. Hata hivyo hawajengi Tabdiy´ yao juu ya Bid´ah, bali juu ya uongo na ujuvi.

4- Haddaadiyyah wa zamani walikuwa wakimfanyia Tabdiy´ Ibn Hajar na an-Nawawiy pamoja na wale wasiowafanyia Tabdiy´. Kuna uwezekano Haddaadiyyah wa leo pia wanafanya hivo, lakini wanatumia Taqiyyah. Jengine ni kuwa watu hawa wanamfanyia Tabdiy´ yule asiyemfanyia Tabdiy´ anayetumbukia katika Bid´ah. Kwa mfano wanawafanyia Tabdiy´ wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah na Salafiyyah wa al-Madiynah na Makkah, Shaykh Ahmad an-Najmiy na Shaykh Zayd al-Madkhaliy. Bali wanawakufurisha baadhi ya wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah. Wanawapiga vita wanachuoni wa Yemen na kuwazungumzia kwa ubaya. Wanawapiga vita wanachuoni wa Algeria na vijana wao. Hawana mawasiliano na Ahl-us-Sunnah ulimwenguni.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kashf Akaadhiyb wa Tahriyfaat wa Khiyaanaat Fawziy al-Bahrayniy, uk. 5-6
  • Imechapishwa: 09/10/2016