5- Wanaiwekea Ahl-us-Sunnah kikomo kwa Haddaadiyyah hawa wapya kwa watu ambao wasiojulikana kwa uongo na ujuvi na kwa watu wasiojulikana waongo kama Fakkaariy, al-Mufarriq, Khaalid al-´Aamiy na watu wengineo wasiojulikana kwa elimu na kusoma. Pamoja na hivyo wanawaita kuwa ni “Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah” na “Ahl-ul-Hadiyth”. Wakati huo huo kila ambaye anawaraddi na kuraddi uongo, ujinga, upotevu na batili yao wanamtuhumu kuwa anawapiga vita Ahl-us-Sunnah.

Kitendo chao hichi ni muendelezo mchafu wa kitendo cha mababu zao, kitendo cha Haddaadiyyah wa mwanzo. Hata na wao pia walikuwa wakisema kuwa pote lao tu ndio Ahl-us-Sunnah na Ahl-ul-Hadiyth na si wengineo. Hata hivyo Haddaadiyyah sio Ahl-ul-Hadiyth was-Sunnah. Bali ni wapinzani wao.

6- Yule mwenye kujiunga na wao anapewa unasibisho wa jina “al-Athariy”. Wao wenyewe wanajiita hivyo. Namna hiyo pia ndivyo wanavyofanya Haddaadiyyah wa leo pale wanapoipa tovuti yao “Athariyyah” na wao wenyewe “Athaariyyuun” na “Ahl-us-Sunnah”.

Mmoja katika viogozi wao ni Fawziy al-Bahrayniy ambaye anajiita mwenyewe kuwa ni “al-Athariy” na wanasarakasi wenzake watafiti “Athariyyah”. Ni katika watu ambao wako mbali kabisa na Athariyyah, mapokezi, wana uelewa mbaya kabisa, matendo na kushikamana na Athariyyah. Ukiongezea juu ya hilo ni kwamba ni katika watu walio na ukweli mdogo kabisa na tabia.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kashf Akaadhiyb wa Tahriyfaat wa Khiyaanaat Fawziy al-Bahrayniy, uk. 6
  • Imechapishwa: 09/10/2016