Baada ya talaka tatu hakuna kumrudi mke


Swali: Nilimtaliki mke wangu mara tatu. Mara ya kwanza ilikuwa wakati wa Maghrib aliponambia maneno yaliyonikasirikisha nikawa nimemtaliki na (baadae) nikamrejea na kumrudisha nyumbani kwa kuwa ni mama wa watoto wangu wawili. Na baada ya siku kukatokea baina yetu magomvi, nikawa nimemtaliki. Akaingia kwangu na kuniomba nimrudi kwa ajili ya (maslahi ya) watoto. Nikamrudisha. Na baada ya siku kukatokea magomvi baina yetu kama ilivyokuwa katika hali ya kwanza na ya pili, nikamtaliki mara ya tatu. Naomba unifaidishe kwa hili.

Jibu: Ni juu yako kurejea mahakamani au Muftiy aliye katika mji wenu waangalie suala hili. Na asli ni kuwa, baada ya Talaka tatu hakuna kurudiana. Lakini apelekewe Qadhiy au Muftiy aangalie hilo. Ama ikiwa uko Saudi Arabia unaweza kuturejelea kwa kutuandikia, ili tuweze kukusaidia wewe na yeye kuyaangalia maudhui hii na tutazame uhakika, wewe, mwanamke na walii wake, mpaka fatwa iwe juu ya jambo la wazi ikiwa uko Saudi. aAma ikiwa uko katika mji mwingine na ikawa unaweza, rejea mahakamani au Muftiy wenu, na In Shaa Allaah Atawafikishwa kutoa fatwa inayoafikiana na Shari´ah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 26/03/2018