Aswali Tahiyyat-ul-Masjid baada ya kuwa ameshaswali Raatibah nyumbani?


Swali 380: Ni ipi hukumu kwa mwenye kuswali Sunnah ya kabla ya Fajr nyumbani kwake kisha akaingia msikitini na akawakuta watu hawajasimama kwa ajili ya swalah. Je, aswali Tahiyyat-ul-Masjid kwa sababu ni miongoni mwa mambo vyenye sababu au abaki akiwa ni mwenye kusubiri bila ya kuswali?

Jibu: Jambo ni lenye wasaa. Akibaki ni mwenye kusimama mpaka kukakimiwa swalah ni sawa. Akikusudia kwa swalah ile Tahiyyat-ul-Masjid na akapenda kubaki akiwa ni mwenye kusimama na asikae chini… kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atapoingia mmoja wenu msikitini basi asikae chini mpaka arukuu Rak´ah mbili.”

pia ni sawa. Akipenda kurukuu Tahiyyat-ul-Masjid na kwayo akanuia Tahiyyat-ul-Masjid pia inafaa. Inazingatiwa ni miongoni mwa vyenye sababu. Allaah ndiye mjuzi zaidi.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 637
  • Imechapishwa: 13/12/2019