Mwanamke wa Kiislamu kujifunua mbele ya mwanamke wa kikafiri

Swali: Ni mambo yepi ambayo mwanamke wa Kiislamu anaweza kuyafunua mbele ya mwanamke wa kikafiri kama mfano wa Ubudha?

Jibu: Maoni sahihi ni kwamba inafaa kwa mwanamke kujifunua mbele ya mwanamke mwenzake. Ni mamoja mwanamke huyo ni muislamu au kafiri. [Kinachofaa kuonekana ni] kile kilicho juu ya kitovu na chini ya goti.  Kuhusu kile kilicho kati ya kitovu na goti ni uchi kwa jinsia zote mbili. Hakitakiwi kuonekana kutoka kwa mwanamke kwenda kwa mwanamke mwenzake. Ni mamoja ni mwanamke wa Kiislamu au asiyekuwa mwanamke wa Kiislamu, ndugu wa karibu au asiyekuwa wa karibu.  Ni kama uchi wa mwanamume kwa mwanamume mwenzake. Inafaa kwa mwanamke kuona kwa mwanamke mwenzake kifua chake, kichwa chake, miguu yake na mfano wa hayo kama mfano wa mwanaume inafaa kwake kuona kwa mwanaume mwenzake kifua chake, miguu yake na kichwa chake.

Kuhusu maoni ya baadhi ya wanachuoni wanaosema kwamba haifai kwa mwanamke muumini kujifunua mbele ya mwanamke wa kikafiri ni maoni yasiyokuwa na nguvu kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanachuoni. Kwa sababu wanawake wa kiyahudi na wanawake wa kishirikina katika kipindi cha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walikuwa wakiingia kwa wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa sababu ya haja zao. Haikuhifadhiwa kwamba walikuwa wakijisitiri kutokamana nao ilihali wao ndio wanawake wachaji na wabora zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (05/39) https://binbaz.org.sa/fatwas/956/%D9%85%D8%A7-%D9%8A%D8%AC%D9%88%D8%B2-%D9%84%D9%84%D9%85%D8%B1%D8%A7%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B3%D9%84%D9%85%D8%A9-%D9%83%D8%B4%D9%81%D9%87-%D8%A7%D9%85%D8%A7%D9%85-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B1%D8%A7%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D9%83%D8%A7%D9%81%D8%B1%D8%A9
  • Imechapishwa: 13/12/2019