Anayesema kuwa ´Aqiydah ni ngumu na kujikakama


Swali: Vipi kumraddi anayesema kwamba ´Aqiydah ni ngumu na kujikakama?

Jibu: Maneno haya ni mabaya ikiwa msemaji amekusudia ´Aqiydah ya Tawhiyd na ´Aqiydah ya waumini. Maneno haya ni kuritadi nje ya Uislamu na kumkufuru Allaah. Maana yake ni kwamba hakuna ndani yake faida inayotambulika na kwamba ni ngumu. Maneno haya ni mabaya na ni kuritadi nje ya Uislamu. Kwa hivyo msemaji ajirudi nafsi yake na amche Allaah na atubu Kwake. ´Aqiydah ndio msingi wa dini; nako ni kule kumwamini Allaah na Mtume Wake, kumwabudu Allaah peke yake, kumtakasia Yeye nia. ´Aqiydah ndio maana ya hapana mungu asiyekuwa Allaah ambayo maana yake ni kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah. Huko ndio kumwabudu Allaah peke yake na kumtakasia Yeye nia. Sambamba na hilo mtu akaacha kumshirikisha, akaamini majina na sifa Zake, akatii maamrisho na kuacha makatazo Yake. Hakuna ugumu katika hayo. Bali yote hayo yako wazi kwa yule ambaye ameongozwa na Allaah na akamuwafikisha kuitafuta haki.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (09/39)
  • Imechapishwa: 11/07/2021