Swali: Ndugu yangu mmoja haswali na ni mtumzima. Mimi na watu wengine wengi tumemnasihi hata hivyo anapuuza swalah sana na ni mara chache sana utamuona anaswali. Wakati mwingine haswali isipokuwa katika Ramadhaan au swalah ya ijumaa peke yake. Tutangamane naye vipi? Je, nimsalimie nitapokutana naye katika kikao au nimkate?

Jibu: Kuacha swalah kwa makusudi ni ukafiri mkubwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Kati ya mtu na shirki na kufuru ni kuacha swalah.”

Ameipokea Muslim katika ”as-Swahiyh” yake.

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Ahadi ilipo kati yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo basi, yeyote atakayeiacha basi amekufuru.”

Ameipokea Imaam Ahmad na watunzi wa “as-Sunan” kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.

Zipo Hadiyth nyingi zenye maana kama hii.

Lililo lazima ni kumnasihi mlengwa na kumbainishia hokumu ya Shari´ah. Akiendelea kuacha swalah basi italazimika kumkata, kuacha kumtolea salamu, kutoitikia mwaliko wake, kwenda kumshtaki kwa mtawala ili kumtaka atubie. Akitubia ni sawa, vinginevyo auliwe. Amesema (Ta´ala):

فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَخَلُّوا سَبِيلَهُمْ

“Lakini wakitubu na wakasimamisha swalah na wakatoa zakaah, basi waacheni huru.”[1]

Hayo yakafahamisha kuwa ambaye hasimamishi swalah basi haachwi huru. Dalili zenye maana kama hiyo ni nyingi.

[1] 09:05

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/268)
  • Imechapishwa: 14/08/2022