Swali: Ndugu wa mume wangu haswali isipokuwa mara chache na mimi naishi na familia ya mume wangu na familia yake hukaa naye hata kama imamu anaswali. Ni kipi kinachonilazimu ilihali mimi sio katika Mahaarim zake? Je, napata dhambi kwa sababu siwezi kumnasihi?
Jibu: Ikiwa haswali basi anastahiki kukatwa, usimsalimie na wala usimuitikie salamu mpaka atubu. Kwa sababu kuacha swalah ni ukafiri mkubwa ijapo hakukanusha ulazima wake kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanazuoni. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Ahadi ilipo kati yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo basi, yeyote atakayeiacha basi amekufuru.”
Ameipokea Imaam Ahmad na watunzi wa “as-Sunan” kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.
Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Kati ya mtu na shirki na kufuru ni kuacha swalah.”
Ameipokea Imaam Muslim katika ”as-Swahiyh” yake.
Lakini akikanusha ulazima wake basi ni kafiri kwa mujibu wa wanazuoni wote. Kwa hiyo ni lazima kwa familia yake wamnasihi na wamsuse asipotubu. Aidha ni lazima kumshtaki kwa mtawala ili amtake kutubu. Akitubia, ni sawa, vinginevyo auliwe. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):
فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَخَلُّوا سَبِيلَهُمْ
“Lakini wakitubu na wakasimamisha swalah na wakatoa zakaah, basi waacheni huru.”[1]

”Nimekatazwa kuwaua wenye kuswali.”
Kwa hiyo hayo yakafahamisha kuwa ambaye haswali haachwi huru. Hapana vibaya kumuua atapoenda kushtakiwa kwa mtawala ikiwa hakutubu.
[1] 09:05
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/284)
- Imechapishwa: 14/08/2022

Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/284)
Imechapishwa: 14/08/2022
https://firqatunnajia.com/vipi-kutangamana-na-shemeji-asiyeswali/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)