Anajutia utovu wa nidhamu aliyomkosea baba yake akiwa mdogo

Swali: Kipindi ambapo nilikuwa na miaka kumi baba yangu alisimama kutaka kunipiga kwa ajili ya jambo fulani na nikaanguka chini. Nikamuombea du´aa mbaya. Matokeo yake akanifukuza na akanipiga. Hivi sasa nina miaka thelathini na baba yangu ameshafariki.

Jibu: Ni lazima kwako kutubu kwa Allaah. Muda wa kuwa ulikuwa bado mdogo kipindi ambacho ´ibaadah haijakuwajibikia hakuna neno juu yako – Allaah akitaka. Lakini mwombee du´aa kwa wingi, msamaha na rehema kama mfano kusema:

اللهم ارحمه، اللهم اجزه عني خيرًا

“Ee Allaah, mrehemu! Ee Allaah, mlipe kheri kupitia kwangu!”

Kipindi hicho ulikuwa huna dhambi kwa njia ya kwamba ´ibaadah zilikuwa hazijakuwajibikia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kalamu imenyanyuliwa kwa watu watatu; aliyelala hadi aamke, mdogo hadi abaleghe na mwendawazimu hadi apate fahamu.”

Wewe kipindi hicho ´ibaadah zilikuwa bazo hazijakuwabikia. Namuomba Allaah akusamehe. Lakini hata hivyo mwombee du´aa kwa wingi.

Check Also

Baba anampiga msichana anamtishia maisha

Swali: Baba yangu anazungumza na mimi kwa ukali, ananipiga na ananitishia kuniua ambapo mume wangu …