Swali: Je, inafaa kwangu kuficha kuwa nimeshaoa kwa ajili ya kumuoa mwanamke wa pili kwa sababu hakuna yeyote anayekubali kumuozesha msichana wake kwa ambaye kishaoa?

Jibu: Hicho ni kitu kinachorejea katika siasa yako wewe. Lakini maoni yangu ni kwamba kila ambavyo mtu atafanya mahusiano yenye nguvu kati yake yeye na mke wake wa kwanza ndio bora kuliko kudhoofisha uhusiano huu. Ukimficha kuwa umeoa atakuja kubainikiwa baadaye. Matokeo yake pengine akaingiwa na kinyongo dhidi yako na pengine akakuadhibu. Kwa sababu mwanamke ndiye mwenye kuaminiwa juu ya mume wake.

Akiwaficha hakuna makatazo kwa mujibu wa Shari´ah. Kuna mwanamme alioa na mke wake wa kwanza hakujua kama alioa mpaka siku ambapo mtoto wa mke wake wa pili alikuja na kuendesha gari. Yeye mwanamke hana haki ya kumkataza.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan al-Ghudayyaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Usrah https://godian.af.org.sa/sites/default/files/2017-10/ftawa-osrh-godian.mp3
  • Imechapishwa: 19/09/2022