Swali: Shari´ah inasemaje juu ambaye anapinga Allaah kuonekana siku ya Qiyaamah?

Jibu: Kuonekana kwa Allaah kumethibiti kwa dalili ya Qur-aan na Sunnah. Amesema (Ta´ala):

لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَىٰ وَزِيَادَةٌ

“Kwa wale waliofanya mazuri watapata [malipo] mazuri kabisa – na ziada.” (10:26)

Wafasiri wa Qur-aan wamesema ´ziada` ni kutazama uso mtukufu wa Allaah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika nyinyi mtamuona Mola wenu kama mnavyouona mwezi usiku wa mwezi mwandamo. Hamtosongamana katika kumuona.”

Kila mmoja atakuwa akimtazama Allaah (Jalla wa ´Alaa) kwa makini.

Hadiyth nyingine inasema:

“Hakuna yeyote katika nyinyi isipokuwa Mola Wake atamzungumzisha. Hakuna baina Yake na yeye mkalimani.”

Atamsogelea karibu na kumkariria madhambi yake ambayo alikuwa akiyafanya duniani ambapo atakubali, kwa sababu hakuna njia ya kukwepa. Allaah (Jalla wa ´Alaa) atamwambia:

“Nilikusitiri duniani na Mimi nakusitiri hii leo.”

Hapana shaka yoyote kuwa mtu ambaye anapinga kuonekana kwa Allaah [Aakhirah] ni kafiri[1]. Kwa sababu anapinga Qur-aan, Sunnah na maafikiano ya wanazuoni. Lakini Allaah amrehemu mtu ambaye anajua kiwango cha nafsi yake. Mtu asiingie katika mambo isipokuwa yale anayoyaweza. Mambo asiyoyaweza ayaache. Lakini baadhi ya watu wanakuwa waovu.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/tofauti-kati-ya-takfiyr-kwa-aina-na-takfiyr-kwa-mtu/

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan al-Ghudayyaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Waqafaat ma´aa Hadiyth tatadaa´ alaykum-ul-Umamu https://godian.af.org.sa/sites/default/files/2017-09/wgfaaat.mp3
  • Imechapishwa: 19/09/2022