Anaamshwa kila siku na kiumbe kuswali usiku

Swali: Kuna mwanamke mwema ambaye anajiwa na mwenye kumuamsha usingizini kila siku katikati ya usiku ili aswali swalah ya usiku. Je, hii inahesabika ni katika karama za mawalii wa Allaah au ni jambo linalotokamana na shaytwaan?

Jibu: Hapana, shaytwaan haamshani kwa ajili ya swalah. Huenda Allaah anamsaidia kupitia kiumbe hicho.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (13) http://alfawzan.af.org.sa/node/2128
  • Imechapishwa: 05/07/2020