Swali: Je, anakufuru mwenye kuacha kufunga midhali anaswali lakini hafungi bila kuwa na udhuru wowote?

Jibu: Mwenye kuacha kufunga hali ya kupinga uwajibu wake ni kafiri kwa maafikiano. Na yule mwenye kuiacha kwa uvivu na uzembe hakufuru. Hata hivyo yuko katika khatari kubwa kwa sababu ya kuacha nguzo miongoni mwa nguzo za Uislamu ambayo kuna maafikiano juu ya uwajibu wake. Mtu huyo anastahiki kuadhibiwa na kutiwa adabu na mtawala kwa mambo yatayomtisha yeye na watu mfano wake. Bali baadhi ya wanachuoni wameonelea kuwa ni kafiri. Ni lazima kwake kulipa siku alizoacha pamoja na kutubu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah al-Qu´uud

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daa’imah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Ladjnah ad-Daa’imah (6060)
  • Imechapishwa: 24/04/2020