Swali: Ni ipi hukumu ya kunywa maji kwa makusudi wakati mtu amefunga pindi mfungaji amehisi uchovu mkubwa? Je, ni lazima kwake kulipa siku hiyo?

Jibu: Mwenye kunywa mchana wa Ramadhaan kwa makusudi funga yake imeharibika. Ni lazima kwake kulipa siku moja badala ya siku hiyo ambayo alikunywa kwa ajili ya uchovu mkubwa.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah al-Ghudayyaan

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daa’imah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Ladjnah ad-Daa’imah (10844)
  • Imechapishwa: 24/04/2020