Ametoa Tasliym kabla ya imamu kwa kusahau

Swali: Ni ipi hukumu ya ambaye anatoa Tasliym kabla ya imamu kwa kusahau? Je, swalah yake ni sahihi?

Jibu: Mswaliji akitoa Tasliym kabla ya imamu hali ya kusahau kisha akazindukana, basi arejee katika nia ya swalah. Kisha baada ya hapo atoe Tasliym baada ya imamu wake na wala hakuna kitu juu yake. Swalah yake ni sahihi. Isipokuwa ikiwa ni mswaliji aliyejiunga kwa kuchelewa. Akiwa amekuja kwa kuchelewa kwa Rak´ah moja au zaidi, basi asujudu sijda ya kusahau baada ya kulipa zile Rak´ah anazodaiwa kwa kitendo chake cha kutoa Tasliym kabla ya imamu kwa kusahau.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/275)
  • Imechapishwa: 01/11/2021